Mbinu za Jinsi Ya Kupata Mtaji wa Biashara Tanzania

Jinsi Ya Kupata Mtaji imekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara walio wengi Asilimia kubwa wanapata wakati mgumu kuendeleza mawazo waliyonayo kutokana na kukosa mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara wanazotaka.

Kuna mbinu ambazo unaweza kutumia ili kupata mtaji kidogo wa fedha ambacho kitakuwezesha kuanzisha biashara yako. Ingawa mtaji sio kigezo pekee cha kufanikiwa katika biashara ila fedha ni kiungo muhimu katika kutekeleza wazo au mradi kwa ufanisi.

Mbinu za jinsi ya kupata mtaji wa biashara

  • Akiba

Akiba ina faida mbalimbali za kujenga mazoea ya kuweka akiba. Ikiwa una fedha kidogo za akiba inakuwa rahisi kuzitumia kama mtaji pale ambapo upo tayari kuanzisha biashara. Akiba inakuwezesha kuchangamkia fursa na kuzifanyia kazi kwa wakati.

Hivyo unaweza kutunza kiasi fulani cha fedha hata kama ni kidogo ili kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako pia Inashauriwa usianze biashara na mtaji mkubwa sana kwani unaweza kupata hasara. Usitumie akiba yako yote kwa wakati moja kama ndiyo kwanza unaanza biashara.

  • Marafiki na Familia

Kama na mahusiano mazuri na ndugu zako unakuwa katika nafasi nzuri ya kuandaa wazo lako la biashara na kuwaomba wakusaidie kupata mtaji ili kuendeleza wazo hilo.

Mara nyingi mtaji wa aina hii baina ya ndugu haina riba, masharti wala vikwazo vya aina yoyote hivyo inakuwa rahisi zaidi kupata. Jambo la muhimu ni kuwa muaminifu na kurejesha fedha ulizopatiwa ndani ya muda mliokubaliana.

  • Taasisi za ujasiriamali

Leo hii kuna taasisi na mashirika mbalimbali yanayotoa mtaji kwa wajasiriamali ili kuwawezesha kutimiza malengo yako Baadhi ya taasisi hizo ni pamoja na Small Starter, Iesc na Afrika Connect.

Hakikisha unafuatilia katika vyombo ya habari pamoja na mitandao ya kijamii au vikundi vya wajasiriamali ili zinapotokea fursa za mtaji upate kuzifahamu na kuzitumia ipasavyo.

  • Taasisi za fedha

Mikopo kutoka taasisi za fedha inaweza kuwa mtaji mzuri wa biashara Kama unataka kupata mtaji kwa njia hii hakikisha umejipanga vizuri na unafahamu mbinu utakazotumia kurejesha mkopo huo.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

2 Comments
  1. Nimewaelewa Sana, kumbe ziko mbinu nyingi Sana za kujiajiri kwa kufanya biashara ya mtaji mdogo tu.
    Je mnayo madarasa mubashara ya kuelimisha kuhusu haya Mambo ya biashara?

Leave a reply