Utangulizi wa Kilimo Bora Cha Matikiti Maji Tanzania

Kilimo cha tikiti maji kimekuwa kikijizolea umaarufu mkubwa hapa nchini na Wakulima wengi zaidi wamekuwa wakihamia kwenye kilimo hiki cha matikiti miaka ya hivi karibuni.

Katika mijadala mbalimbali ya fursa za kilimo, kilimo cha matikiti ni nadra sana kukosekana.

Hapa Tanzania soko la tikiti maji ni zuri kipindi cha joto ambapo walaji wengi hupendelea tunda hili kutokana na hali ya hewa ya joto.

Wauzaji wa matikiti katika masoko wanadai  kuwa biashara ya tikiti ni nzuri sana wakati wa joto na hudorora katika nyakati za baridi.

Taarifa kama hizo ni nzuri sana kwa mkulima mjasiriamali anayelenga uhitaji wa soko kwani anakuwa na mipangilio mizuri katika uzalishaji wake ili asipate hasara.

Pia ni kilimo cha muda mfupi kwani huchukua miezi miwili hadi mitatu kiasi kwamba mkulima anaweza kulima hadi mara nne kwa mwaka mmoja.

Kilimo cha tikiti maji kinafanyika katika eneo lenye udongo laini usio na mabonge kwani mbegu zake hupandwa moja kwa moja shambani.

Pia shamba linapaswa kuwa katika eneo la wazi lisilo na miti sababu vivuli vya miti vinaweza kupelekea matikiti yasitoe matunda.

Uchaguzi wa aina ya mbegu ni kitu cha msingi sana katika kilimo hiki kwani shughuli zote zinajengwa kwenye msingi huo. kama ukikosea kuchagua aina ya mbegu basi kilimo chako cha matikiti maji hakitakuwa na tija.

Kuchagua mbegu nzuri na zenye ubora za matikitimaji sio kazi rahisi, wakulima wengi hukimbilia mbegu maarufu ambazo zinatangazwa zaidi ambapo mara nyingi wanapokwenda kwenye uhalisia kwa kulima mbegu hizo wanakumbana na matokeo tofauti.

Takribani asilimia tisini ya tikiti maji ni maji hivyo yanahitaji maji mengi ili kukua vizuri. Hivyo kabla ya kufanya aina hii ya kilimo hakikisha una uhakika wa maji kipindi chote cha ukuaji.

Matunda ya matikiti huitaji maji kipindi chote mpaka hatua ya uvunaji. Mizizi ya mmea wa tikiti huenda chini sana kutafuta maji kwa ajili ya kusaidia matunda yenye ukosefu wa maji.

Mkulima anatakiwa kumwagilia mimea maji ya kutosha Kama kiwango cha maji hakiridhishi basi hata matunda hayo hayawezi kukua kama inavyotakiwa.

Subscription Form

Tuandikie email yako uweze kupata post za mtandao wa wauzaji kwa haraka.

Tuandikie Mawazo Yako

Leave a reply